5 Oktoba 2025 - 15:10
Sheikh Hemed Jalala na Sheikh wa Mkoa wa Tabora (BAKWATA) waonyesha: Matendo ya Hekima Yanayounganisha Watu na Kuimarisha Umoja wa Kiislamu

Kwa hakika, ziara hii ni kielelezo cha Uislamu wa kweli uliofundishwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w.) - Uislamu wa upendo, udugu, na umoja. Kama alivyonena Imam Ali (a.s.): "Kuweni walinganizi wa watu bila kutumia maneno yenu, bali kwa matendo yenu.” (Nahjul-Balagha, Hikma 31)

Sheikh Hemed Jalala na Sheikh wa Mkoa wa Tabora (BAKWATA) waonyesha: Matendo ya Hekima Yanayounganisha Watu na Kuimarisha Umoja wa Kiislamu

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-
Tarehe 04 Oktoba, 2025 / Tabora - Tanzania, Katika mwendelezo wa ziara yake ya Kidini katika maeneo mbalimbali ya nchi, Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna Ashari Tanzania (T.I.C), Maulana Sheikh Hemedi Jalala Mwakindenge, akiambatana na jopo lake la Tabligh kutoka Jijini Dar es Salaam, alifanya ziara maalum ya kidini Mkoani Tabora.

Katika ziara hiyo, Sheikh Jalala alipata fursa ya kumtembelea nyumbani kwake Sheikh wa Mkoa wa Tabora (BAKWATA), Sheikh Ibrahim Mavumbi.

Sheikh Hemed Jalala na Sheikh wa Mkoa wa Tabora (BAKWATA) waonyesha: Matendo ya Hekima Yanayounganisha Watu na Kuimarisha Umoja wa Kiislamu

Mazungumzo baina ya viongozi hao wawili yalijikita katika kuimarisha Umoja wa Kiislamu, kudumisha amani ya kitaifa, na kukuza upendo na mshikamano kati ya Waislamu wa Madhehebu zote nchini Tanzania.

Kwa upande wake, Sheikh Mavumbi alionesha furaha na shukrani kubwa kwa ugeni huo, akiahidi ushirikiano wa karibu na viongozi wa Kishia waliopo Mkoani humo katika juhudi za pamoja za kuimarisha udugu wa Kiislamu na amani ya kijamii.

Sheikh Hemed Jalala na Sheikh wa Mkoa wa Tabora (BAKWATA) waonyesha: Matendo ya Hekima Yanayounganisha Watu na Kuimarisha Umoja wa Kiislamu

Umoja wa Kiislamu katika Mwanga wa Qur’an Tukufu 
Mafundisho ya Qur’ani Tukufu yanaweka wazi wajibu wa Waislamu kushikamana na kamba moja ya Mwenyezi Mungu. Allah (s.w.t.) anasema:

"وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِیعًا وَلَا تَفَرَّقُوا"

Shikamaneni wote kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu, wala msifarakane.” (Aal Imran, 3:103).

Aya hii inasisitiza kuwa nguvu ya Waislamu ipo katika umoja wao. Ziara kama hii ya Sheikh Jalala ni kielelezo cha utekelezaji wa amri hii tukufu — kushikamana kwa Waislamu wote kwa msingi wa Qur’an na Sunna.

Sheikh Hemed Jalala na Sheikh wa Mkoa wa Tabora (BAKWATA) waonyesha: Matendo ya Hekima Yanayounganisha Watu na Kuimarisha Umoja wa Kiislamu

Mtume (s.a.w.w.) na Wito wa Upendo na Mshikamano
Mtume Muhammad (s.a.w.w.) amesema:

"الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ، لَا يَظْلِمُهُ وَلَا یَخْذُلُهُ وَلَا ."

“Mwislamu ni ndugu wa Mwislamu mwenzake; hamdhulumu, hamtelekezi, wala hamdharau.”

Maneno haya matukufu yanaonyesha wajibu wa kila Mwislamu kulinda heshima na utu wa mwingine. Ziara ya Sheikh Jalala na Sheikh Mavumbi ni mfano hai wa utekelezaji wa mafundisho haya ya Mtume (s.a.w.w.) katika zama zetu.

Sheikh Hemed Jalala na Sheikh wa Mkoa wa Tabora (BAKWATA) waonyesha: Matendo ya Hekima Yanayounganisha Watu na Kuimarisha Umoja wa Kiislamu

Amani na Maelewano: Msingi wa Jamii ya Kiislamu
Qur’ani inabainisha wazi kuwa Waislamu wanapaswa kuwa vinara wa amani:

"وَإِنْ جَنَحُوا لِلسَّلْمِ فَاجْنَحْ لَهَا"

Na wakielekea amani, nawe elekea nayo.”(Al-Anfal, 8:61)

Kwa msingi huu, juhudi za viongozi wa Kiislamu nchini — kama walivyofanya Sheikh Jalala na Sheikh Mavumbi — zinachangia katika kudumisha amani, maridhiano, na ustawi wa kitaifa.

Kwa hakika, ziara hii ni kielelezo cha Uislamu wa kweli uliofundishwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w.) - Uislamu wa upendo, udugu, na umoja. Kama alivyonena Imam Ali (a.s.):

"Kuweni walinganizi wa watu bila kutumia maneno yenu, bali kwa matendo yenu.” (Nahjul-Balagha, Hikma 31).

Sheikh Hemed Jalala na Sheikh wa Mkoa wa Tabora (BAKWATA) waonyesha: Matendo ya Hekima Yanayounganisha Watu na Kuimarisha Umoja wa Kiislamu

Kwa matendo yake ya hekima na upendo, Sheikh Jalala amekuwa mfano hai wa mwalimu wa amani na mshikamano kwa jamii ya Kiislamu nchini Tanzania.

Sheikh Hemed Jalala na Sheikh wa Mkoa wa Tabora (BAKWATA) waonyesha: Matendo ya Hekima Yanayounganisha Watu na Kuimarisha Umoja wa Kiislamu

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha